Sunday, January 22, 2017

HOW TO CLEAR YOUR LOCAL DISK FULL

HOW TO CLEAR YOUR LOCAL DISK FULL









Umejaza filamu na nyimbo kibao katika diski yako, labda ni magemu pia. Tamthilia je? Inaweza ikawa moja ya vitu hivi au ni mambo mengine kibao yamejaa kwenye kompyuta yako kiasi ya kwamba inakuwa ni vigumu ata pa kujua mafaili makubwa ya kufuta ni yapi hasa.

Unaangalia kompyuta yako na inakuambia diski C yako inakaribia kujaa kabisa na hivyo unatakiwa ufute baadhi ya mafaili, ila ndio hivyo tena kutokana na jinsi yalivyomengi hufahamu mafaili yapi ni makubwa au yapo wapi hayo makubwa kutokana na wewe kuwa na mafolda mengi kwelikweli. Leo tunakutambulisha kwa programu moja ya bure kwa watumiaji wa kompyuta/laptop za Windows, inaitwa WinDirStat.
Ndio kuna njia zingine za kupunguza nafasi katika diski yako kama vile kutumia programu wa Windows ifahamikayo kama ‘Disk Cleaner’, ila hiyo haikuoneshi mafaili yako mwenyewe. Yenyewe inasaidia mafaili ya system ya kompyuta tuu.
Programu ya WinDirStat inakupa uwezo wa kufahamu mafaili gani ni makubwa na ni kwa ukubwa gani na pia inakupa uwezo wa kuyafuta kwenda kwenye ‘Recycle Bin’ au kuyafuta moja kwa moja kabisa bila kupitia Recycle Bin.
Pia kwa kutumia rangi mbalimbali utaoneshwa mafaili muhimu ambayo si vizuri uyaguse
Pia kwa kutumia rangi mbalimbali utaoneshwa mafaili muhimu ambayo si vizuri uyaguse
Unaweza kushusha WinDirStat bure kabisa hapa -> http://www.fosshub.com/WinDirStat.html

Available link for download